Back to top

Kijana mmoja ahukumiwa jela miaka 20 kwa udhalilishaji wa mtoto, Lindi

08 February 2019
Share

Mahakama ya wilaya ya Lindi, imemuhukumu Salumu Kunyumu miaka 26, mkazi wa kijiji cha Milola B, kifungo cha miaka 20 jela baada ya kukutwa na hatia ya kosa la udhalilishaji kwa mtoto wa miezi mitatu  kinyume na kifungu cha 138 C kubwa ya sheria ya kanuni ya adhabu ya sura ya 16 marejeo ya mwaka 2002.

Akizungumza na ITV ofisini kwake wakili wa serikali na mwendesha mashtaka mkuu wa mkoa wa Lindi, Juma Maige, amesema hukumu hiyo ilitolewa na hakimu wa mahakama ya wilaya ya Lindi, Franco Kiswaga na  hukumu hiyo imetolewa ili iwe fundisho kwa watu wengine  ambao wana tabia kama hizi kukomesha vitendo ambavyo wamekuwa wakifanya hasa kwa watoto.

Kwa kumujibu wa wakili Maige amesema siku hiyo ya tukio mama  wa mtoto huyo alimuomba jirani yake amwangalie mwanae na kwenda kisimani kuchota maji ndipo alipotumia nafasi hiyo.

Hata hivyo wakili Maige amewataka wananchi mkoani Lindi kuwalinda watoto wao na kuhakikisha hawatendewi vitendo vya ukatili na watoto wa kike wapate elimu ya kupambana na mimba za utotoni.
+
Kwa upande wake mkuu wa mkoa wa Lindi, Bw.Godfrey Zambi,ameipongeza mahakama ya wilaya ya Lindi kwa kutoa hukumu bila kuchelewesha.