Back to top

Kimbunga “Michael” chatarajia kulikumba jimbo la Florida

10 October 2018
Share

Kimbunga kilichopewa jina la Michael kinatarajiwa kulikumba jimbo la Florida nchini Marekani jioni ya leo huku mamlaka zinazohusika na masuala ya hali ya hewa zikionya kuwa kimbunga hicho kitasababisha mvua kubwa maeneo ya ukanda wa pwani .

Watu wapatao 375,000 wanaoishi katika ukanda wa pwani wa Jimbo la Florida wametakiwa kuyahama makazi yao ili kuepusha madhara kwani kwa mujibu wa kituo kinachohusika na masuala ya vimbunga nchini humo(NHC) madhara ya kimbunga Michael yatakuwa makubwa ambayo hayajawahi kutokea katika eneo hilo.