Back to top

Kinababa wanaonyonya maziwa ya wake zao chanzo utapiamlo kwa watoto.

07 August 2020
Share

Tabia ya baadhi ya wanaume kunyonya maziwa ya wake zao wenye watoto wachanga nyakati za usiku warudipo nyumbani kwa madai kuwa wanakata ulevi imetajwa kuwa ni chanzo cha ongezeko la watoto wenye udumavu na utapiamlo wilayani Shinyanga.

Hayo yamebainishwa na afisa lishe wa halmashauri ya wilaya ya Shinyanga wakati wa kilele cha wiki ya unyonyeshaji watoto wilayani humo iliyofanyika katika kijiji cha mwalukwa wikayani humo.

Nao baadhi ya wakazi wa wilaya hiyo wakiwamo wanawake wanaonyonyesha wameeleza jinsi maelekezo ya wataalamu wa afya juu ya lishe kwa watoto wachanga yalivyosaidia huku baadhi ya wanaume wakionyesha baadhi ya mboga lishe za kienyeji wanazotumia kuboresha afya kwa wanawake waliojifungua pamoja na watoto wachanga.

Kwa upande wake mganga mfawidhi wa halmashauri ya wilaya ya shinyanga Dkt.Mamelta Basike amekiri kuwepo kwa changamoto hiyo licha ya taasisi mbalimbali binafsi na za serikali kuendelea kutoa elimu kwa jamii hiyo juu ya changamoto zinazosababisha udumavu na utapiamlo kwa watoto.

 

Picha na Maktaba.