Back to top

Kipanga aagiza kukamatwa mkandarasi wa ujenzi chuo cha ualimu Mpwapwa

25 January 2021
Share

Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe.Omary Kipanga ameagiza kukamatwa kwa mkandarasi na wasimamizi wa mradi wa ujenzi wa majengo matano mapya katika chuo cha ualimu Mpwapwa baada ya kushindwa kutekeleza maagizo yaliyotolewa awali.

Mhe.Kipanga ametoa maagizo hayo katika ziara yake ya kukagua utekelezaji wa ujenzi wa chuo hicho ambapo amelazimika kumweka ndani Mkurugenzi wa Kampuni CF Builders ya jijini Mwanza, Fredy Chacha na wasimamizi wa mradi huo Mhandisi Laurent Vicent na Thobias Ntobi baada ya kushindwa kutoa sababu zilizo sababisha kutotekeleza maagizo aliyoyatoa Disemba 19, 2020 na kusababisha mradi huo kusuasua.