Back to top

Kisanduku cha kunakili taarifa za safari za ndege chapatikana.

11 March 2019
Share

Kisanduku cheusi (Black Box) cha kunakili taarifa ya safari ya ndege ya Ethiopian Airlines iliyoanguka mjini Bishoftu Kilomita 60 Kusini Mashariki mwa mji mkuu Addis Ababa siku ya Jumapili, kimepatikana.

Taarifa zinaeleza kwamba kampuni ya ndege ya Ethiopian imethibitisha kwamba 'black box' kimepatikana ila kimeharibika kidogo.

Kampuni ya kutengeneza ndege ya Boeing ilioko Marekani inakabiliwa na maswali baada ya ndege hiyo kuanguka dakika sita baada ya kupaa na kusababisha vifo vya watu 157.