Back to top

Kiwanda bubu cha kuchenjulia dhahabu chakamatwa Kahama.

01 January 2020
Share

Waziri wa Madini Dotto Biteko akishirikiana na ofisi ya madini ya wilaya ya Kahama amefanya msako katika maeneo ya kuchenjulia dhahabu wilayani Kahama na kufanikiwa kukamata kiwanda bubu kinachotumika kuchenjua dhahabu  kilichoko katikati ya makazi ya watu katika kitongoji cha Bunango.

Akizungumza baada ya kusaka na kukamata kiwanda hicho ambacho wamiliki wake wametoroka na kujificha Waziri Biteko amesema licha ya serikali kuweka mazingira mazuri kwa wachimbaji wa madini kufanya kazi zao bila kusumbuliwa bado kuna baadhi yao wanakiuka utaratibu hali ambayo inahatarisha maisha ya wananchi.

Hata hivyo viongozi wa kata,kijiji na kitongoji wametofautiana kauli juu ya uwepo wa kiwanda hicho hali ambayo Waziri Biteko ameitilia mashaka na kuagiza baadhi yao kushililiwa na jeshi la polisi.