Back to top

Kiza cha tanda Mauaji ya mama na mwanae wilayani Hai.

21 April 2019
Share

Wazee wa kimila wa jamii ya wafugaji wa kimasai wa wilaya ya Hai wameliomba jeshi la polisi kuvitumia vyombo vyake vyote vya uchunguzi wakiwemo mbwa kuwatamabua watu waliohusika na mauaji ya kinyama ya wanawake wawili wa jamii hiyo kwa kunyongwa kutokana na mgogoro wa ardhi.

Mwenyekiti mstaafu wa wazee hao malaigwanani mzee Kinokore Laisungu wa mtaa wa Lerai amesema, migogoro ya ardhi si utamaduni wa jamii hiyo uliosababisha vifo vya wanawake hao Koini Lembile na Mwanae Neema Mollel wa mtaa wa Lerai na kuiomba serikali ichukue hatua kali kukomesha kitendo hicho kisijirudie tena.

Mtoto wa marehemu Bwana.Ibrahimu Molle amesema, marehemu mama yake alikuwa na mgogoro wa ardhi ya ekari saba tangu mwaka 2014 na mtu mmoja aitwaye Paul Kivamba ambaye anashikiliwa na jeshi la polisi kwa tuhuma za mauaji hayo.

Akizungumza na ITV kwa njia ya simu kamanda wa polisi mkoani Kilimanjaro Kamanda Hamisi Issa amethibitisha kuwepo kwa mauaji hayo ambayo marehemu walinyongwa ndani ya nyumba yao kata ya bondeni huku marehemu neema akikutwa na kamba shingoni ambayo ilitumika katika tukio hilo.