Back to top

Kiza watuhumiwa kuchanganywa na wafungwa, Naibu waziri afafanua.

13 September 2019
Share

Serikali imekiri kuwa katika baadhi ya magereza nchini hususani magereza yenye mahabusu suala la kuwatenganisha wahalifu kwa kuzingatia vigezo vya umri kosa na kifungo limekuwa halizingatiwi japo sheria inaelekeza hivyo.

Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe.Hamad Masauni alipokuwa akijibu swali la Mhe.Naja Murtaza mbunge wa viti maalum aliyetaka kujua kwa nini serikali inawachanganya watuhumiwa na wafungwa.

Mhe.Masauni amesema moja wapo ya jukulu la jeshia la Magereza ni kuwapokea na kuwahifadhia  magereza wahalifu wa aina zote wanaopelekwa kwa mujibu wa sheria kanunia na taratibu za nchi.

Ameongeza kuwa pamoja na jukumu hilo kanuni za uendeshaji wa magereza za mwaka 1967 zinaelekeza  kuwa uhifadhi wa wahalifu magerezani utafanyika kwa kuzingatia tenganisho kwa kigezo cha jinsia umri kosa na kifungo.

Hata hivyo Naibu huyo akasema kuwa kanuni na taratibu za magereza zinakataza na zinatoa adhabu  kwa mhalifu endapo atabainika kufanya makosa mbalimbali ambayo atayafanya makosa akiwa  gerezani.