Back to top

Kongamano la kukanyaga mafuta Moshi, watu 20 wamefariki,16 mahututi.

02 February 2020
Share

Watu 20 wamefariki dunia wakati wakipambana kukanyaga mafuta ya upako kwenye kongamano la Mtume Boniface Mwaiposa huku wengine 16 wakikimbizwa hospitali ya rufaa ya mkoa wa Kilimanjaro ya Mawenzi .

Jeshi la polisi linawashikilia watu Saba kwa mahojiano na wanaendelea kumtafuta Mtume Boniface Mwamposa,kufuatia vifo vya watu Ishirini katika kongamano la kukanyaga mafuta Moshi.

Mpaka sasa Miili 14 kati ya 20 waliofariki jana usiku kwenye kongamano la kukanyaga mafuta ya upako yatambulika majeruhi 16 waendelea na matibabu.


Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro amesema Anna Mgwira Ibada ya pamoja ya kuwaaga kufanyika kesho katika uwanja wa Majengo mkoani Kilimanjaro lilipofanyika kongamano hilo.