Back to top

Korea Kaskazini,Eritrea zina idadi kubwa ya watu walioko katika utumwa

20 July 2018
Share

Utafiti wa shirika moja la kutetea haki za binadamu umebaini kuwa Korea Kaskazini na Eritrea zina idadi kubwa zaidi ya watu walioko katika utumwa.

Ripoti ya mwaka wa 2018 kuhusu Viwango vya Utumwa Duniani iliyochapishwa na shirika la haki za binaadamu la Walk Free Foundation imesema Burundi pia ina kiwango kikubwa cha utumwa.

Utafiti huo unazingatia mchango wa migogoro na ukandamizaji wa serikali katika utumwa mamboleo.\

Imesema katika nchi hizo tatu, serikali inawalazimisha watu kufanya kazi bila malipo, ambapo watu wake wenyewe wanafanyishwa kazi kwa manufaa yake yenyewe.

Kwa mujibu wa makadirio ya shirika la Walk Free Foundation na Shirika la Kimataifa la Kazi, zaidi ya watu milioni 40 waliishi utumwani kote duniani kufikia mwaka 2016.