Back to top

Kubenea na Komu wavuliwa nyadhifa ndani ya CHADEMA isipokuwa Ubunge

18 October 2018
Share

Kamati kuu ya chama cha demokarasia na maendelo CHADEMA iliyoketi kuwajadili  wabunge wawili wa chama hicho Mhe.Saed Kubenea mbunge wa Ubungo na Mhe.Athony Komu mbunge wa Moshi vijijini imewavua nyadhifa zote walizonazo katika chama isipokuwa ubunge baada ya kubakia kuwa wamefanya vitendo ambavyo ni vya utovu wa nidhamu.

Akizungumza na waandishi wa habari naibu katibu mkuu wa chama hicho bara na mbunge wa Kibamba Mhe. John Mnyika amesema  kamati hiyo imefikia maamuzi  mbalimbali ikiwemo kuwavua nyadhifa zao sambamba  na kuwataka waombe radhi.

Katika mkutano huo na waandishi wa habari Mhe. Kubenea alisema  anaomba radhi kwa chama na watanzania wote.

Naye  Mhe. Komu amekishukuru chama kwa jinsi kilivyochukua jambo hilo na kulipa uzito hadi kufikia hapo  na anaomba radhi.

Tarehe 13/10 mwaka huu ilisambaa clip ya sauti iliyoanzia kundi la whatsap kanda ya kaskazini ikihusisha mazungumzo ya   Komu na Kubenea hivyo kufuatia kusambaa kwa ujumbe huo wenye maudhui ya kuashiria utovu wa nidhamu kamati kuu ya chama iliitisha kikao maalum kuwajadili wabunge hao ambao walihojiwa kwa saa kadhaa kabla ya kamati hiyo  haijafikia maamuzi  hayo.