Back to top

'Kuku wa kisasa hawana madhara kiafya'-Ulega.

16 November 2018
Share

Serikali imesema kuku wa kisasa hawana madhara kiafya kwa wanadamu kama ambavyo baadhi ya watu wamekuwa wakisema.

Naibu Waziri wa wizara ya mifugo na uvuvi Abdalah Ulega amesema hayo bungeni mkoani Dodoma wakati akijibu maswali yaliyoelekezwa kwa wizara yake.

Naibu Waziri wa wizara ya mifugo na uvuvi Abdalah Ulega.

Naibu Waziri Ulega amesema dawa na vyakula ambavyo vinatumika kwa kuku hao vimekuwa vikifanyiwa utafiti na vimebainika kuwa na ubora unaostahili.

Bungeni hapo baadhi ya wabunge walionesha hofu yao kuhusiana dawa na vyakula wanavyokula kuku hao kuwa vimekuwa vikileta mabadiliko hasi kwa baadhi ya walaji wake.