Back to top

Kumbukizi ya mwaka mmoja wa ajali ya lori yafanyika Morogoro.

10 August 2020
Share

Vilio, majonzi na simanzi vimetawala katika makaburi ya kola wakati wa kumbukizi ya mwaka mmoja wa watu waliopoteza maisha katika ajali ya lori la mafuta lililopinduka na kuwaka moto katika eneo la Msamvu mkoani Morogoro mwezi Agosti mwaka jana na kusababisha vifo vya watu 115.

Marehemu waliopoteza maisha wamezikwa katika makaburi ya Kola mkoani Morogoro ambapo kumbukizi hiyo  imeanza kwa dua na sala kutoka kwa viongozi wa dini.

Maombolezo hayo yamehudhuriwa na viongozi mbalimbali wa serikali, vyama vya siasa na vyombo vya ulinzi na usalama vya mkoa wa Morogoro ambao wamewasisitiza wananchi kutoa taarifa za majanga na kuchukua tahadhari wakati wa matukio ya aina hiyo.

Mkuu wa mkoa wa Morogoro Loata Ole Zanare ametoa pole kwa wananchi  waliopoteza ndugu zao huku akiviagiza vyombo vya ulinzi na usalama kuendelea kuchua hatu kwa watu wanaokiuka sheria za usalama barabarani.