Back to top

Kumi wakamatwa kahama kwa kufanya biashara ya dhahabu nyumbani.

19 July 2019
Share

Wizara ya madini inawashikilia watu zaidi ya 10 wakazi wa eneo la Kakola wilayani Kahama Mkoani Shinyanga wakituhumiwa kufanya biashara bubu ya dhahabu majumbani mao ikwemo kusafirisha nje ya nchi bila kulipa ushuru na kodi ya serikali.

Msako huo ulioongozwa na waziri wa madini Mhe.Dotto Biteko pia umegundua baadhi ya mitambo ya kuchenjulia dhahabu ambayo awali ilifungiwa kwa kufanya udanganyifu wa kuwaibia wachimbaji wadogo wanapofikisha udongo wenye dhahabu kuchenjua kiujanja.

Aidha  baadhi ya watendaji wa ofisi ya wizara ya madini wa wilaya ya Kahama wamehusishwa na udanganyifu wa  kuweka rakili  bandia baada ya kukata rakili halisi .

Kamishna wa tume ya madini Profesa Abdulkarim Mruma akawataka wachimbaji wadogo kuheshimu fursa waliyopewa na Mh.rais Magufuli kwa kuchimba kihalali na kuacha kukwepa kulipa kodi.