Back to top

Kuoga kunavyoweza kukupunguzia hatari ya kupata magonjwa ya moyo.

25 March 2020
Share

Kitendo cha binadamu kupata muda mzuri wa kuoga maji ya moto ( kinaweza kumuepusha kupata magonjwa ya moyo kwa asilimia 28,na mshituko (Stroke) kwa asilimia 26.

Kufuatia utafiti mpya uliochapishwa Machi 24,2020 katika  Journal heart uliohusisha raia wa Japan 61,000 wenye magonjwa ya moyo baada ya kufuatilia maisha ya watu hao kwa miaka 20,majibu ya utafiti huo ni kutokana na uhalisia wa kwamba kila mtu anapooga anapunguza hatari ya presha ya juu ya damu.

Lakini pia umuhimu mwingine wa kuoga maji ya moto ni kupunguza kiwango cha mafuta mwilini (burn calories) ,maji ya moto yanasaidia kupata usingizi kwa haraka ,kuweka misuli sawa, ni mazuri kwa afya ya ngozi  na huifanya ngozi kuwa laini,utengeneza mzunguko mzuri wa damu mwilini,husaidia kuondoa maumivu ya kichwa na pia hufanya miili yetu kujisikia vizuri.