Back to top

Leornard Manyama ajitosa kuwania Urais kupitia CHADEMA.

09 July 2020
Share

Leonard Toja Manyama amejitokeza kuchukua fomu ya kugombea Urais kupitia chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).

Bwana Manyama ni mwalimu na mtaalam wa mipango miji, kauli mbiu yake niamini nikuvushe.

Ameeleza vipaumbele alivyonavyo endapo atakuwa Rais wa Tanzania kuwa.

"Atairejesha Rasimu ya Katiba iliyooendekezwa na Jaji Warioba, naamini yale ndio maoni ya Watanzania, Watanzania ndio wanaotakiwa waamue nchi iendeshwe vipi"

"Nitafuta Sheria ya vyombo vya habari ambayo imekuwa msumari katika uandishi wa habari, nitahakikisha sheria hii kandamizi inaondolewa" 

"Katika siku 100, nitarekebisha fao la kujitoa, sio wengine wawapangie wengine maisha yao na pesa zao walizozifanyia kazi"

Manyama Anakuwa mwanachama wa tano kuchukua fomu hiyo ya kugombea Urais kupitia chama hicho.