Back to top

Likizo za kawaida kwa watumishi zafutwa Kigoma.

16 December 2018
Share

Likizo zote za kawaida kwa watendaji wa serikali pamoja na wakuu wa wilaya katika mkoani Kigoma zimefutwa  hadi watumishi hao watakapo hakikisha tatizo la upungufu wa vyumba vya madarasa 358 vilivyosababisha zaidi ya wanafunzi elfu 12 kukosa nafasi ya kuanza masomo ya kidato cha kwanza kwa mwaka 2019 linamalizika.

Kaimu katibu tawala mkoa wa Kigoma Mhandisi Aziz Mtabuzi amesema kila kiongozi na mtumishi wa serikali anatakiwa kuhakikisha vyumba vya madarasa vinapatikana jitihada pia zinazotakiwa kuungwa mkono na taasisi, mashirika pamoja na wananchi.