Back to top

Lissu aahidi kuboresha maisha ya wavuvi mwambao mwa ziwa Victoria.

27 September 2020
Share

Mgombea Urais wa Tanzania kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA ), Tundu Lissu ameahidi kuboresha maisha ya wananchi wanaoishi na kujishughulisha na sekta ya uvuvi katika mwambao mwa ziwa Victoria.

Akihutubia mkutano wa kampeni katika kijiji cha Bwai Kumsoma maarufu kama 'Bwai Paris' wilayani Musoma, mgombea Urais huyo wa Tanzania, ametoa rai kwa wananchi kuongozwa na hekima na busara katika kumchagua kiongozi bora ambaye ataondosha changamoto walizonazo.

Kisha msafara wa mgombea Urais huyo kwa tiketi ya CHADEMA ukaelekea eneo la Sirari jimbo la Tarime Vijijini ambako Lissu amelakiwa na umati wa wananchi barabarani.