Back to top

Lissu akiwa Rais wa Tanzania kupunguza madaraka ya Rais.

19 September 2020
Share


Mgombea Urais wa Tanzania kwa tiketi ya CHADEMA Tundu Lissu amewaomba wananchi wa mkoa wa Kigoma kuongoza harakati za vyama vya upinzani kwa kuchagua mgombea atakayeweza kukiondoa chama cha mapinduzi madarakani katika uchaguzi mkuu ujao.

Akihutubia mkutano wa kampeni za chama hicho kuelekea uchaguzi mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani katika viwanja vya Mwanga Centre manispaa ya Kigoma/ Ujiji, mgombea Urais huyo kwa tiketi ya CHADEMA akionekana dhahiri kumpigia kampeni mgombea ubunge wa jimbo la Kigoma mjini kupitia chama cha ACT Wazalendo Zitto Zuberi Kabwe.

Tundu Lissu amezungumzia suala la katiba mpya, huku akiweka agano na Watanzania kwa kusema iwapo akichaguliwa kuingia madarakani atapunguza madaraka ya Rais.