Back to top

Lissu:Ni wajibu wa serikali kusaidia wananchi wake.

21 September 2020
Share

Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo ( CHADEMA ) Mh.Tundu Lissu ameendelea na safari yake ya kutafuta kura kwa Watanzania katika wilaya za mkoa wa Kagera kwa kuhaidi kuondoa mageti barabarani ambayo yamekuwa kikwazo kwa wakulima wa mazao na wafugaji.

Akihutubia mkutano wa kampeni katika uwanja wa Kokoto, Mgombea urais huyo amesema ni wajibu wa serikali kuwasaidia wananchi wake misaada ya kiutu na kibinadamu pindi yanapotokea majanga ya asili kama tetemeko la ardhi lililotokea mkoani Kagera mwaka 2017 .

Aidha, Mgombea urais huyo wa CHADEMA Tundu Lissu amefanya mikutano mingine ya kampeni zake katika wilaya ya Kyerwa pamoja na mjini Kayanga wilayani Karagwe.