Back to top

Lugola:Ni bodaboda za makundi 3 ndio zitakamatwa na kupelekwa vituoni.

20 May 2019
Share

Waziri wa mambo ya ndani Mhe.Kangi Lugola amepiga marufuku ukamataji holela wa pikipiki ambazo zimekuwa zikivunja sheria za usalama barabarani ambazo hukamatwa na kupelekwa katika vituo vya polisi.

Akijibu swali Mbunge wa viti maalum Rehema Juma
waziri Lugola amebainisha aina ya makosa ambayo yatahusisha pikipiki kukamatwa na kupelekwa kituoni,kundi la kwanza ni bodaboda ambayo imehusika kwenye uhalifu,pili ni bodaboda inayohusika na kesi(kuhusika kwenye ajali barabarani au iliyoibiwa),tatu ni bodaboda ambayo haina mwenyewe,

Waziri Lugola amesema pikipiki zingine zozote ambazo haziko kwenye makundi hayo kama vile uvaaji wa kofia ngumu,side mirrors na uvunjaji wa sheria zingine za usalama barabarani hakuna kupelekwa kituo cha polisi bali zitapigwa faini.