Back to top

Maafisa Mikopo vyuo vya elimu ya juu wawashiwa taa nyekundu.

19 October 2019
Share

Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi Na Teknolojia, Mhe.William Ole Nasha amewaonya Maafisa Mikopo wa vyuo vya elimu ya juu,  kuacha mara moja tabia ya kugeuka mawakala ili kushughulikia matatizo ya mikopo kwa wanafunzi kwa kuomba fedha kwa ajili ya kazi hiyo.

Naibu Waziri Ole Nasha amesema hayo Mjini Morogoro wakati wa kikao kazi baina ya menejimenti ya Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya juu nchini, na Maafisa Mikopo wa vyuo vya elimu ya juu nchini na amewasisitiza maafisa hao kuacha tamaa za kutaka malipo ili kushughulikia matatizo ya wanafunzi.

Naibu Katibu Mkuu katika Wizara hiyo anayeshughulikia Sayansi na Elimu ya Juu, Prof.James Mdoe, amesema serikali haitawavumilia wanaochelewesha wanafunzi kupata mikopo kwa namna yo yote.