Back to top

Maambukizi mapya 117 ya virusi vya Corona yathibitishwa Kenya.

19 June 2020
Share

Wizara ya Afya nchini Kenya imethibitisha maambukizi mapya 117 ya virusi vya Corona katika muda wa saa 24 zilizopita na kufikisha jumla ya wagonjwa 4374 waliothibitishwa kufikia sasa.

Naibu Waziri wa Afya Dkt Rashid Aman akidokeza kuwa maambukizi mpya ni ya raia 112 wakenya na raia watano wa kigeni ambao wizara ya afya inasema kuwa haitoweka bayana uraia wao kutokana na mwafaka na mataifa jirani ya kenya kutofanya hivyo.

Wizara ya Afya imethibitisha kuondoka hospitalini kwa wagonjwa  91 na kufikisha waliopona kufikia 1550 hata hivyo idadi ya vifo imefikia 119 baada ya watu 2 zaidi kuaga dunia kutokana na COVID 19 nchini Kenya.