Back to top

Maambukizi ya Corona Kenya yazidi kuongezeka.

06 May 2020
Share

Kenya imepiga marufuku ya kuingia na kutoka katika mitaa ya Eastleigh jijini Nairobi na Old Town huko Mombasa kwa siku 15 zijazo baada ya wizara ya afya kusajili visa vipya 47 vya maambukizi mapya  ya virusi vya corona na kufikisha 582 idadi ya waliopatikana kuwa na virusi hivyo kufikia sasa.

Visa 32 vikiripotiwa huko Mombasa,Nairobi visa 11 visa 2 katika kaunti ya Busia,Kiambu 1 na Kwale.

Hatua ya kenya kutangaza marufuku ya  kuingia na kutoka katika mitaa ya Eastleigh na Old Town ikifuatia ongezeko la maambukizi katika mitaa hiyo.

Waziri wa afya Mutahi Kagwe akitangaza kuwa biashara zote zitasalia kufungwa.Idadi ya waliofariki aidha imeongezeka na kufikia 26 baada ya watu 2 zaidi kufariki huko Mombasa.

Aidha Kenya imeripoti kupona kwa watu 8 zaidi na kufikisha watu 190 waliopona.

Wakenya wakiombwa kusalia ndani kwa ndani ili kuzuia kuenea zaidi kwa virusi vya Corona.