Back to top

Maambukizi ya Corona yafikia 1477 Kenya.

27 May 2020
Share

Kenya imetangaza wagonjwa wapya  123 wa virusi vya Corona hii ikiwa idadi kubwa zaidi ya maambukizi ya virusi vya Corona katika muda wa siku moja na kufanya idadi ya jumla kufikia 1477 hadi sasa.

Waziri wa afya Mutahi Kagwe anasema kuwa wagonjwa hao  wamethibitishwa baada ya watu 3077 kupimwa.

Maambukizi ya hii leo yakiwa ni pamoja na 85 jijini Nairobi na 24 kaunti ya Mombasa.

Wizara ya afya aidha imethibitisha kufariki kwa watu watatu zaidi na kufikisha waliofariki kufikia 55 hadi sasa.

Kenya vilevile imedokeza kuwa miongoni mwa wagonjwa walioko hospitalini 7 wako katika chumba cha wagonjwa mahututi,wanne wakiwa kwenye ventileta na 3 wakiwa wameekewa gesi ya oxygen.