Back to top

Maambukizi ya Corona yafikia 3727 Kenya.

15 June 2020
Share

Idadi ya maambukizi ya virusi vya Corona nchini Kenya imeongezeka na kufikia watu 3727 hii ni baada ya Wizara ya afya kuthibitisha maambukizi mapya 133 ya Covid-19 katika muda wa saa 24 zilizopita.

Idadi ya waliopona imefikia 1286 baada ya watu wengine 33 kupona na kuondoka hospitalini.

Idadi ya vifo kutokana na homa ya Corona imefikia 103 baada ya mtu mmoja  kufariki.

Sampuli 3365 zilipimwa katika muda wa saa 24 zilizopita.