Back to top

Maambukizi ya Corona yapungua kwa siku 3 mfululizo.

16 February 2020
Share

China leo imeripoti kupungua maambukizi mapya ya virusi vya Corona kwa siku ya tatu mfululizo wakati ikibainika kuwa uongozi wa taifa hilo ulifahamu ukubwa wa tishio la virusi hivyo hata kabla ya kutolewa kwa tahadhari.

Tume ya afya ya China imesema kumekuwa na matukio mapya 2,009 pekee upande wa China Bara na kufanya idadi ya walioambukizwa virusi hivyo kufikia Elfu-68 na 500.

Kiwango cha vifo hakijapungua baada ya kurekodiwa vifo vipya 142 na kufikisha idadi ya waliokufa kutokana na ugonjwa huo kuwa watu 1,665.

Mlipuko wa virusi vya Corona ulianzia kwenye mji wa Wuhan uliopo katikati ya jimbo la kati ya China la Hubei.