Back to top

Mabadiliko ya teknolojia yakwamisha TAKUKURU.

18 April 2019
Share

Taasisi ya kuzuia na kupambana na Rushwa (TAKUKURU) imesema mabadiliko ya technolojia yamekuwa moja ya kikwazo cha kazi zao kwani  wafanyaji wa makosa yanayohusiana na rushwa wamekuwa wakibadilisha mbinu za ufanyaji wa makosa hayo hivyo wamekuwa wakitoa elimu kwa watendaji wao ili kuendana na mabadiliko hayo.

Hayo yamezungumzwa na Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU Diwani Athumani katika mazungumzo maalum na ONLINE ITV ambapo pia amesema baadhi ya mashahidi wa keshi za rushwa wamekuwa wakishindwa kuonyesha ushirikiano pale kesi inapofika mahakamani hivyo kukwamisha mwenendo wa matukio mengi ya rushwa.

Hata hivyo Diwani amesema wamekuwa wakipokea taarifa za matukio ya rushwa lakini tukifatilia tunakuta hayako sawa.

Usikose kufuatilia kipindi cha Dakika 45 ambacho kinaruka kila Jumatatu kuanzia saa Tatu kamili Usiku kupitia ITV Tanzania,Radioone na Capital radio kufahamu mengi kupitia TAKUKURU.