Back to top

Mabondia Ruvuma waomba wadhamini katika mapambano ya ngumi.

14 June 2020
Share

Mabondia wa mkoa wa Ruvuma wameomba wadau na serikali kuwaunga mkono kwa kuandaa mapambano ya ndondi  na kuwasaidia vifaa vya ngumi ili kukuza mchezo huo mkoani humo.

Wanamasumbwi hao wametoa ombi hilo wakati wakijifua na mazoezi makali ilhali hawana uhakika wa mapambano ya ngumi  kwa kuwa hakujakuwa na mapambano hayo mkoani Ruvuma kwa miaka mitatu.
 
Kwa upande wake aliyewahi kuwa bondia nambari moja  kwa ubora nchini kwa vijana katika uzito wa kati Musa Chitepete amesema anaamini misaada ya wadau na serikali itasaidi kuinua ngumi mkoani Ruvuma.