Jopo la watalaam wa mifugo na madaktari bingwa wa wanyama mkoani Arusha wameanza kutoa matibabu ya bure kwa wanyamakazi aina ya punda kihongo wenye vidonda na majeraha makubwa kwenye miili yao inayotokana na kubebeshwa mizigo mizito bila matibabu huku wafugaji wakisema hawaoni sababu ya kumtibu mnyama huyo kwani si kwa matumizi ya kitoweo.
Watalaam hao wa mifugo wanasema wameamuwa kutoa huduma ya matibabu ya bure baada ya kuguswa na mateso wanayoyapata wanyama hao ambao hivi sasa wanatishio la kutoweka baada ya kukithiri kwa wizi wa wanyama hao huku baadhi ya waliowahi kupatiwa elimu ya ufugaji bora wa punda wakieleza walivyobadilika baada ya elimu hiyo.
Watetezi wa haki za wanyama wanasema wanaishukuru serikali kwa kuunga mkono juhudi zao katika utetezi wa wanyama kazi ambao utumikishwa bila kupatiwa haki ya kutibiwa.