Back to top

Madereva 8 watanzania wakutwa na Corona mpakani .

14 May 2020
Share

Madereva 8 raia Watanzania  wamerejeshwa nyumbani baada ya kukutwa na virusi vya Corona baada ya kupimwa katika maeneo ya mipakani ya  Namanga na Isebania.

Madereva Saba wamethibitishwa kuwa na virusi hivyo katika eneo la Namanga na mmoja katika eneo la mpakani mwa Kenya na Tanzania la Isebania.

Naibu Waziri wa Afya Dk Mercy Mwangangi aidha anasema kuwa Kenya haina nia ya kufunga mipaka yake na mataifa mengine ya Afrika Mashariki licha ya maambukizi ya mipakani kuongezeka.

Wizara ya afya ikithibitisha kuwa maambukizi ya virusi vya Corona nchini Kenya yamefikia 758 baada ya watu 21 zaidi kuthibitishwa kuwa na virusi vya Corona baada ya sampuli 1486 kupimwa katika muda wa saa 24 zilizopita.

Aidha idadi ya waliofariki imeongezeka na kufikia 42 baada ya watu wawili zaidi kufariki hapa Nairobi.

Vilevile idadi ya waliopona imefikia 284 baada ya watu wengine 3 kupona na kuondoka hospitalini.