Back to top

Madereva wa Serikali vinara wa kuendesha magari kwa mwendokasi waonywa

07 November 2018
Share

Serikali imewaonya madereva wa Serikali ambao wamekuwa  vinara wa kuendesha magari kwa mwendokasi na kusababisha ajali ambazo zimekuwa zikishamiri  katika siku  hivi karibuni.

Naibu Waziri wa Mambo ya ndani Hamad Masauni ametoa onyo hilo bungeni mkoani  Dodoma wakati akijibu maswali yaliyoelekezwa kwa wizara yake na kuongeza kuwa sheria ni msumeno lazima hilo litekelezeke.

Amewataka maaskari wa usalama barabarani kuwakamata madereva wa namna hiyo na kuwaweka mahabusu na kisha kuwafikisha mahakamani ili wawe funzo kwa madereva wengine.

Naibu Waziri Masauni amewataka viongozi wa taasisi za umma kuwakemekea madereva wanaoendesha magari kwa mwendokasi kutokana na athari ambazo wamekuwa wakisababisha ikiwemo vifo na uharibifu wa magari pindi ajai inapotokea.