Back to top

Madereva wafanyiwe mafunzo ya kujihami kupambana na ajali- Silanda

05 November 2018
Share

Meneja Usalama Barabarani na Mazingira SUMATRA Bw.Geoffrey Silanda amesema kuna uhitaji zaidi wa madereva kufanyiwa mafunzo ya kujihami ili kuweza kupambana na ajali za barabarani nchini ambazo kwa asilima kubwa zimekuwa zikichangiwa na makosa ya kibinadamu.

Akizungumza wakati wa kufunga mafunzo ya kujihami kwa madereva Bw.Geoffrey amesema mafunzo hayo ni sehemu ya mapendekezo ya kamati iliyoundwa kufanya uchunguzi wa ajali mbali mbali zinazotokea na hivyo kupendekeza madereva kutoka kampuni hizo wafanyiwe mafunzo ya kujihami.

Naye mkuu wa idara ya usalama katika usafirishaji na mafunzo ya mazingira chuo cha taifa cha usafirshaji Bibi Mary Makyao amewataka madereva kubadili tabia wakubadili kuelimika na kuendesha kwa kujihami.