Back to top

Maduka 10 yafungiwa kwa kosa la kuwauzia wakulima mbegu feki Mbeya.

05 December 2018
Share

Zaidi ya maduka 10 ya kuuza pembejeo za kilimo mkoani Mbeya yamefugwa na taasisi ya kudhibiti ubora wa mbegu(TOSCI) baada ya kukutwa yakiwauzia wakulima mbegu feki.

Maofisa wa TOSCI, wamefanya ukaguzi wa kushtukiza katika mikoa ya Mbeya na Songwe ambako wamekagua zaidi ya maduka 130 na kati yake maduka 10 yamefugiwa kuendelea na biashara hiyo baada ya kukutwa yakiuza mbegu feki na mengine yakiwa hayakusajiliwa kwa mujibu wa sharia.