Back to top

Maduka ya saruji Magu yaliyokiuka bei elekezi yafungwa.

17 November 2020
Share

Wauzaji wa saruji wilayani Magu mkoani Mwanza wameiomba serikali kuangalia chanzo cha kupanda kwa bei ya bidhaa hiyo na ichukue hatua za kudhibiti mfumuko huo ili wananchi wasiendelee kununua saruji kwa bei kubwa, huku baadhi ya maduka yaliyokiuka bei elekezi ya serikali yakifungwa kwa muda usiojulikana.

Wafanyabiashara hao wa saruji mjini Magu wanatoa ombi hilo baada ya Mkuu wa wilaya hiyo Salum Kali kuendesha msako kwenye maduka ya saruji ili kuwabaini wauzaji walioamua kupandisha bei ya bidhaa hiyo kinyume cha utaratibu.