Back to top

Mafundi simu wote nchini kusajiliwa rasmi.

05 December 2018
Share

Serikali imeanzisha mpango wa kuwasajili mafundi simu wote kote nchini ili kutambulika katika mfumo rasmi wa mawasiliano ikiwa ni mpango mkakati kudhibiti matumizi mabaya ya simu kwa kuwatambua mafundi wanaofanya kazi hizo kwa njia halali ya usajili.
 
Mpango huo wa kusajili mafundi wote kwa mujibu wa sheria umetangzwa jijini Dar es salaam naibu katibu mkuuu wa sekta ya mawasiliano Wizara ya ujenzi uchukuzi na mawasiliano Dokta Jim Yonazi.