Back to top

Mafuriko yaua watu sita  Aude kusini magharibi mwa Ufaransa.

15 October 2018
Share

Watu sita wamepoteza na wengine kadhaa kukwama kwenye nyumba katika eneo la Aude kusini magharibi mwa Ufaransa baada ya kutokea mafuriko yaliyosababishwa na mvua iliyonyesha kwa saa chache.

Miongoni mwa watu 6 waliopoteza maisha kwa kuzolewa na maji ni pamoja na mtawa mmoja.

Kiongozi wa eneo hilo Alain Thirion anasema kuwa watu wengi wameshindwa kutoka katika nyumba zao na hasa walio kwenye ghorofa na hivyo wanafanya jitihada za kupata ndege ya kuwaondoa kwenye nyumba zao.

PICHA:Sky News.