Back to top

Mahakama 26 kati ya 68 za Mwanzo hazifanyi kazi mkoani Tanga

03 February 2020
Share

Jumla ya mahakama 26 za mwanzo kati ya 68 zilizopo mkoani Tanga hazifanyi kazi kutokana na uchakavu mkubwa wa majengo yake na hivyo kusababisha sehemu kubwa ya wananchi katika maeneo mbalimbali hasa sehemu za vijijini kuhangaikia huduma hiyo.

Akizungumza katika uzinduzi wa mahakama ya mwanzo ya kisasa iliyojengwa katika tarafa ya Magoma wilayani Korogwe,jaji mfawidhi mahakama kuu kanda ya Tanga Mheshimiwa Amiry Mruma amesema jitihada zinafanywa ili kuhakikisha wanazikarabati ili huduma za kisheria ziweze kutolewa katika maeneo hayo

Katika uzinduzi wa mahakama hiyo inayaotarajiwa kuhudumia wakazi zaidi ya 58,000 waliopo katika tarafa ya Magoma,mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama wilayani Korogwe Kisa Gwakisa ametoa rai kwa wadau wa mahakama kuharakisha mashauri ili kuleta maendeleo katika uwekezaji 

Kufuatia hatua hiyo mwenyekiti wa baraza la ardhi wilayani Korogwe amelalamikia changamoto zinazoikabili sekta hiyo na kuiomba serikali kuharakisha kuzitatua ili kuondoa malalamiko kutoka kwa wananchi