Back to top

Mahakama Kuu Tanzania yatupilia mbali pingamizi za Mwanasheria Mkuu

13 February 2019
Share

Mahakama Kuu ya Tanzania imetupilia mbali pingamizi za Upande wa Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG) kwenye kesi ya kikatiba inayopinga Wakurugenzi kusimamia Uchaguzi.

Shauri hilo ambalo lilikuwa kwa Jaji Atuganilwe Gwala limetolewa maamuzi leo.

Uamuzi huo unatokana na Serikali kuwasilisha pingamizi kupitia hoja zao wakidai shauri hilo lilifunguliwa kinyume na sheria kutokana na kuwepo kwa mapungufu katika hati ya kiapo.

Pia katika hoja zao wamedai kuwa shauri hilo halikuwa na maana yoyote, hivyo inaomba mahakama isiipe kipaumbele.

Katika maamuzi yake Jaji Gwala amesema anatupilia mbali pingamizi hizo za serikali, Kutokana na maamuzi hayo ya Mahakama Kuu, shauri hilo linasubiri kupangiwa Majaji kwa ajili ya kuanza kusikilizwa.

Shauri hilo lilifunguliwa na Bob Wangwe akipinga Wakurugenzi wa Halmashauri kusimamia chaguzi za kiasiasa huku akiwa na Wakili wake Fatma Karume.