Back to top

Mahakama nchini Afrika kusini yakataa rufaani ya Zuma

30 November 2019
Share


Mahakama nchini Afrika kusini imekataa rufaani iliyowasilishwa na rais wa zamani Jacob Zuma ambao ilitaka kuzuia kushitakiwa kwake kwa madai ya rushwa kuhusiana na mkataba wa ununuzi wa silaha wenye thamani ya dola bilioni 2.

Hukumu hiyo inafungua njia kwa kesi hiyo  iliyokuwa ikisubiriwa kwa muda mrefu dhidi ya Zuma kuanza Februari 2020.

Zuma aliyekuwa madarakani tangu mwaka 200 hadi 2018, aliwahi kukata rufaa akitaka kufutwa kabisa kwa mashitaka hayo 18 ya udanganyifu, ulanguzi na utakatishaji fedha kuhusiana na mkataba huo wa ununuzi wa silaha na kampuni la Ufaransa la kutengeneza silaha la Thales katika miaka ya 1990.

Katikati ya mwezi Oktoba, mahakama kuu ya Pietmaritzburg ilitupilia mbali shauri lililoletwa mahakamani na Zuma na Thales kutaka kutosikilizwa kabisa kwa kesi hiyo.