Back to top

Mahakama ya Kisutu yahamia Tume ya Madini

12 September 2018
Share

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es salaam imelazimika kuhamia katika ofisi za Tume ya Madini kuona ushahidi wa kesi ya madini inayowakabiliwa washitakiwa Aazam Uddin Nazim raia wa India na Ango Mbossa ambaye ni mtanzania wanaotuhumiwa kukutwa na madini aina ya rough gemstone yenye thamani ya zaidi ya shilingi bilioni nne , Januari  Mosi mwaka 2017 Jijini Dar es Salaam.