Back to top

Mahakama yaamuru ushahidi wa video kesi ya viongozi CHADEMA kuonyeshwa

19 August 2019
Share

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, imeamuru kuonyeshwa kwa video iliyopokelewa mahakamani hapo kama ushahidi katika kesi ya uchochezi inayowakabili viongozi tisa wa Chadema, akiwemo Mwenyekiti wake, Freeman Mbowe, ionyeshwe .

Uamuzi huo umetolewa  Agosti 19, 2019 na Hakimu Mkazi Mkuu wa Mahakama hiyo, Thomas Simba, baada ya kupitia hoja za upande zote mbili.

Uamuzi huo unatokana na upande wa utetezi kupinga video hiyo isionyeshwe mahakamani hapo kutokana na upande wa mashtaka kushindwa kuandaa mazingira wezeshi.

Akitoa uamuzi huo, Hakimu Simba alisema sababu zilizotolewa na upande wa utetezi haina mashiko, hivyo video hiyo inatakiwa ionyeshwe katika ukumbi wa Tehama uliopo katika mahakama ya Kisutu.

Hata hivyo hakimy huyo ameiairsha  kesi hiyo kwa muda wa dakika 20 kwa ajili ya maandalizi ya kuangalia video.


Itakumbukwa kuwa , Julai 26, 2019, upande wa utetezi ulipinga kuonyesha kwa mkanda wa video uliotolewa na upande wa mashtaka mahakama.

Wakili wa washtakiwa hao,Peter Kibatala alidai kuwa upande wa mashitaka ulipaswa kuandika barua kwa uongozi wa mahakama kuomba kutumika kwa kituo cha mafunzo kuonesha maudhui  yaliyopo katika mkanda huo wa video.