Back to top

Mahakama yamsomea mashtaka ya ubakaji mtuhumiwa akiwa hospitali.

11 January 2019
Share

Mahakama ya hakimu mkazi mkoa wa Mara imelazimika kuhamia katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Mara mjini Musoma,kwa ajili ya kumsomea shitaka la ubakaji mkazi mmoja wa kijiji cha Butiama anayedaiwa kukatwa ulimi wake kwa meno wakati wa tukio hilo.

Akisomewa shitaka hilo la ubakaji akiwa katika wodi namba sita katika hospitali ya rufaa mkoa wa Mara,mbele ya Hakimu mkazi Mfawidhi wa mahakama ya mkoa wa Mara Mh Rahim Mushi,mwendesha mashitaka wa serikali  Frank Nchanila,amesema mtuhumiwa huyo Mathias Magembe Nyambereka mwenye umri wa miaka 23 anadaiwa kutenda kosa hilo Januari sita majira ya saa sita na nusu usiku.

Amesema mtuhumiwa huyo akijifanya ni mwendesha pikipik maarufu kama bodaboda,walikula njama na wenzake wawili kisha kumbeba binti huyo na baada ya kufika vichakani walitenda tukio hilo ndio mtuhumiwa akang’atwa