Back to top

Maombi ya kuzuia mchakato wa kumuondoa Meya Iringa yagonga mwamba.

27 March 2020
Share

Mahakama ya mkoa wa Iringa imetupilia mbali maombi ya kuzuia mchakato wa kumuondoa madarakani Meya wa Manispaa ya Iringa Alex Kimbe.
 
Akitoa maamuzi hayo Hakimu mkazi wa Mahakama ya mkoa wa Iringa Aden Kanje amesema maombi yaliyowasilioshwa yalikosewa na hivyo kuifanya mahakama hiyo kushindwa kuisikiliza kesi hiyo kwa kujibu wa sheria.