Back to top

Mahakimu watakiwa kuhakikisha wanatoa hukumu za Haki.

26 February 2021
Share

Jaji Mkuu wa Tanzania Profesa Ibrahim Juma amewataka Mahakimu wakazi nchini kuhakikisha wanatoa hukumu za haki kwa wananchi na kupunguza misongamano ya kesi mahakamani.

Akiwaapisha Mahakimu Wakazi sabini jijini Dar es Salaam pia amewataka wakubali kufanya kazi katika vituo wanavyopangiwa na wasitarajie kupangiwa kazi mijini, kwani maeneo mengi ya vijiji hayana wataalam hao wa sheria.

Mwenyekiti wa Chama cha Majaji na Mahakimu Wanawake Tanzania amesema ongezeko la majaji na Mahakimu wanawake ni ishara ya uzingatiaji wa usawa katika kuwapata watendaji wa vyombo vinavyotoa maamuzi.