Back to top

Majeruhi wa ajali ya gari Arumeru wapewa rufaa

22 April 2019
Share

Majeruhi wawili kati ya watano katika ajali ya magari iliyotokea jana katika eneo la Oldonyosambu wilayani Arumeru na kusababisha vifo vya watu wawili wamehamishiwa kwenye hospitali ya rufaa ya Arusha Medical Center baada ya hali zao kuzidi kuwa mbaya huku kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Arusha Jonathan Shana akitoa onyo kali kwa madereva wanaotumia siku za sikukuu kuendesha magari kwa mwendo kasi bila kuchukua tahadhari