
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Philip Mpango amesema Serikali inatambua umuhimu wa sekta binafsi kama kichocheo cha kuimarisha sekta ya utalii hapa nchini hivyo imekuwa ikichukua hatua mbalimbali za kuleta mageuzi hususani katika sheria na maboresho ya sera ya bajeti ili kusaidia ukuaji wa sekta hiyo.
Makamu wa Rais amesema hayo wakati wa ufunguzi wa onesho la sita la kimataifa la utalii la Swahili (Swahili International Tourism Expo) linalofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Mlimani City Jijini Dar es salaam.
