Back to top

Makamu wa Rais aitaka AALCO kuimarisha ushirikiano.

21 October 2019
Share

Makamu wa Rais Mhe.Samia Suluhu Hassan ameitaka Jumuiya ya Ushirikiano ya Sheria za Kimataifa kati ya nchi za Asia na Afrika (AALCO)kuendelea kuimarisha ushirikiano katika kutekeleza sheria za kimataifa kati ya Asia na Afrika kwa upande wa biashara za kimataifa, uwekezaji na usalama.

Akifungua Mkutano wa Kimataifa wa Jumuiya ya Ushirikiano ya Sheria za Kimataifa kati ya nchi za Asia na Afrika (AALCO) Mhe.Samia amesema katika kufikia malengo na mafanikio katika viwango vya kimataifa nchi wanachama wa AALCO hazina budi kusimama pamoja kwa kushauriana.

Akizungumza katika mkutano huo, Waziri wa Katiba na Sheria Balozi Augustine Mahiga amesema katika mkutano huo wa 58 Tanzania imejipanga kuja na ajenda mbalimbali ikiwemo kuwekewa vikwazo kwa Zimbabwe pamoja na mfumo wa biashara kati ya nchi za AALCO na nchi zilizoendelea.

Awali Rais wa Jumuiya ya Ushirikiano ya Sheria za Kimataifa kati ya nchi za Asia na Afrika (AALCO) balozi Koji Haneda amesema Jumuiya ya Ushirikiano ya Sheria za Kimataifa kati ya nchi za Asia na Afrika (AALCO) inafanya kazi nzuri katika kupata rasilimali kwa ajili ya maendeleo endelevu katika sheria za Kimataifa.