Back to top

Makamu wa Rais aitaka sekta binafsi kuwekeza katika lugha ya kiswahili

15 February 2019
Share

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh Samia Suluhu Hassan ameitaka sekta binafsi kuwekeza katika lugha ya kiswahili kwa kuhakikisha inakua, inaendelezwa na kulindwa ili Tanzania inufaike zaidi na lugha hiyo.

Makamu wa Rais ameyasema hayo katika  hafla ya utoaji wa tuzo ya kiswahili kwa waandishi wa fasihi wa Afrika  yaliyofanyika jijini Dar es salaam, na kuongeza  kuwa uwekezaji katika lugha  ya kiswahili kutaleta maendeleo ya biashara zetu na taifa kwa ujumla.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa bodi ya wadhamini wa tuzo  hiyo Dkt Abdullatif Abdallah amesema lengo la shindano hili ni kuwapa ari waandishi na wazungumzaji wa lugha ya kiswahili kuendeleza kutumia lugha hiyo.