Back to top

Makamu wa Rais akutana na Watanzania waishio Ivory Coast.

03 November 2022
Share

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Philip Mpango, amewaasa watanzania waishio nchini Ivory Coast, kuendelea kuitangaza vema Tanzania, kuvutia wawekezaji  na wao kuchangamkia fursa za uwekezaji katika sekta mbalimbali nchini. 

Makamu wa Rais ameyasema hayo, baada ya kukutana na kufanya mazungumzo na watanzania hao katika Jiji la Abidjan, ambapo pia amewasihi kuendelea kusaidia kwa karibu ndugu na jamaa, wenye uhitaji katika familia zao nchini Tanzania kwa kutumia mifumo rasmi ya utumaji kifedha.